Msanii wa bongo fleva aliye wahi kutamba na nyimbo ya vaileth,ametoa lawama zake kwa bahadhi ya wasanii wa bongo flavour.akiongea na BONGO5 matonya ameyasema haya
“Mimi napenda kuwapongeza wasanii wote wazuri ambao wanafanya vizuri
lakini kuna watu pia hawastahili kupongezwa kwa sababu wamekuja
kuuharibu muziki wetu,” alisema Matonya. “Kwahiyo wanaokuja kwa matusi
kwa nia ya kuuharibu muziki tutawachukia sana,”Aliongeza,“Kuna watu wamekuja kuuharibu muziki wa bongofleva. Kwa sababu tunaona kabisa kuna watu ambao walikuwa hawana ajira wamepata ajira. Sisi ambao tumefanya muziki huu kwa muda mrefu tumeona mafanikio pamoja na connection. Lakini kuna watu ambao hawajiwezi wanakuja na wanafanikiwa kwenye muziki, kwahiyo tukiwaruhusu kuuharibu muziki wetu kwa njia yoyote watakuwa wameharibu chakula cha watu wengi,”
msanii huyu pia ameachia kibao kinachokwenda kwa jina la MR LEGEZA KIDOGO
0 coment�rios: